Natural Bliss

116. JINSI YA KUOSHA NYWELE ASILI KIRAHISI/KUZUIA ZISIKATIKE

Tunajua kwamba nywele kukatika ni changamoto ya watu wengi hasa wenye nywele za asili. Nywele kukatika kunachangiwa na vitu au mambo mbali mbali mojawapo ikiwa kutokutumia njia sahihi za kuosha nywele.

Leo tutaangalia namna ambavyo unaweza kuzuia nywele kukatika hasa ukiwa kwenye process za kuosha nywele zako; watu wanaotunza nywele zao za asili wanaita 'WASH DAY'.

🧚‍♂️Kama umesuka Fumua nywele zako kwa uangalifu ili zisikatike.

-Hapa unaweza kuchanganya maji na mafuta halafu ukaweka kwenye spray bottle ukanyunyizia kuanzia kwenye ngozi ya kichwa, kuzipa nywele pamoja ngozi unyevu, halafu ndio ufumue

-Ukimaliza kufumua detangle nywele zako kwa utaratibu usitumie nguvu, kama kuna nywele zimejifunga tumia leave in conditioner au product ambayo inateleza 'slippery state' kufungua (unaweza tumia rojo la bamia au aloevera' kirahisi tu zinaachana.

🧚‍♂️Siku moja kabla inaweza kuwa usiku kabla ya kulala zipe nywele unyevu, unaweza kupaka mafuta pia kwenye ngozi ya kichwa halafu twist au suka mabutu makubwa makubwa.

-Pia unaweza fanya hot oil treatment pia inasaidia kustimulate ukuaji wa nywele.

🧚‍♂️Vaa satini cap halafu lala

🧚‍♂️Wakati wa kuosha nywele sasa hakikisha umeloanisha nywele zote zimejaa maji kabla ya kupaka shampoo, pindi unapopaka shampoo yako nywele iwe mbichi kabisa (Tumia shampoo isiyo na viambata sumu kabisa, kama vile sulphates, parabens na minerals etc)

🧚‍♂️Unaweza tumia maji ya vugu vugu mwanzoni baada ya kumaliza process unasuuza na maji ya baridi ili kufunga pores.

🧚‍♂️Ukimaliza kushampoo nywele zako twist out (fumua mabutu ulisuka) halafu suuza nywele vizuri.

🧚‍♂️Baada ya hapo unaweza kufanya steaming/protein treatment kama una ratiba hiyo.

🧚‍♂️Halafu fuata process ya LCO kuweka unyevu kwenye nywele zako.

L - Leave in conditioner

C - Cream

O - Oil /Mafuta

Tupigie au Whatsap: 0672765929 kwa mahitaju ya bidhaa mbalimbali za nywele

Post a Comment

0 Comments