Deep conditioning ni process ya kutibu nywele ama kuimarisha nywele kwakutumia moisturizers special za kufanya hivyo au protein treatment based conditioners. Kwa hiyo protein treatment ni aina ya deep conditioner maana deep conditioner zipo za aina nyingi aina moja wapo ndio hiyo protein treatment.
HAIR MASK pia ni aina ya deep conditioner ambayo pia husaidia kutibu nywele zilizoharibika, zilizokosa nuru na kutokukua. Kiufupi deep conditioner na hair mask ni almost kitu kimoja sema tu zina utofauti mdogo sanaa ila ni vitu vile vile tu.
🌸Tofauti kati ya deep conditioner na hair masks ni kwamba deep conditioner hufanya kazi hasa hasa ya kufanya nywele ziwe soft na Hair mask kazi yake ni kufanya nywele ziwe na strength yaani ziwe strong.
So ufanyaji either wa hair mask au deep conditioner unategemea na hitaji la mtu husika.
🧚♂️Kama nywele zako ni ngumu, kavu, hazipendezi basi pendelea sana kufanya deep conditioner .
🧚♂️Na kama nywele yako haina afya, inakatika katika, yaani haina nguvu ipo ipo tu basi kila week pendelea kuifanyia hair mask.
Kumbuka hizi zote zinaboost Hair Growth yaani zinafanya pia nywele zikue na ziwe na afya. Na pia hazina utofauti kihivyo. Ukifanya hair mask ni kama umefanya deep conditioner na ukifanya deep conditioner ni kama umefanya hair mask, inategemea tu una shida gani unataka kuitatua.
INAENDELEA...
0 Comments