Moja kati ya matatizo mengi ambayo yanawakumba watu wanaopenda nywele zao (hasa natural hair/nywele asili) ni kukatika (breakage).
🧚♂️Hapa tuelewane kitu kimoja, kwanza kuwa na nywele asili sio tatizo ila tatizo kubwa ni jinsi tunavyozitreat au kuzitunza nywele zetu.
🧚♂️Nywele huweza kukatika kwa sababu ya mambo ya hormone (kwa cases chache) lakini 90% inatokana na jinsi tunavyozihandle.
Inaweza kusababishwa na;
🌺Aina ya msuko unaosuka
🌺Aina ya bidhaa unazotumia kama zina viambata sumu
🌺Kitambaa unachofunga au kuvaa
🌺Hali ya hewa na aina ya maji ya sehemu husika
🌺Vitu unavyokula/Chakula
🌺Kutokunywa maji ya kutosha
🌺Kutumia moto mara kwa mara
Njia unazoweza kutumia ili kuzuia au kupunguza tatizo hili;
Kabla ya kutafuta njia ya kuondoa tatizo kwanza inatakiwa kutambua chanzo cha tatizo taratibu kama vile unavyotafuta chanzo cha allergy, mwishoni lazima utagundua chanzo cha nywele zako kukatika.
💐hakikisha nywele zako zina unyevu (well moisturised) wakati wote.
💐Zingatia aina ya misuko, nywele isivutwe sana na kupewa pressure kubwa (ngozi ya kichwa irelax)
💐Tumia LOC method kila unapoosha nywele zako.
💐Epuka kutumia moto mara kwa mara.
ITAENDELEA....
0 Comments