📌Maji ya baridi yanaongeza mng’ao wa nywele yako. 🧚♂️Yanasaidia kufunga cuticles za nywele/ vishina na kufanya cuticles zilaliane juu ya zingine ambayo inaipa nywele yako muonekano soft na unaong’aa.
📌Inapunguza nywele kujisokota baada ya kuoshwa, na kuzuia kukamaa kwa nywele (reduction of frizz)
📌Yanasaidia kuondoa mba (dandruff)
📌Maji ya baridi pia yanahamasisha mzunguko wa damu mzuri kwenye ngozi ya kichwa (scalp) ambayo inachochea ukuaji wa nywele yako.😊
🧚♂️Ukiosha nywele kwa maji ya moto unaondoa natural oils za nywele yako na kupunguza natural moisture (unyevu) wa nywele zako.
🧚♂️Hii inaacha scalp yako ikiwa kavu sana (dehydrated) pia nywele zinajisokota na kukamaa.
🧚♂️Maji ya baridi yanaseal moisture (kutunza au kuzuia kupoteza unyevu wa nywele) ambayo inaacha scalp yako ikiwa hydrated vizuri 😊.
🧚♂️Yanasaidia pia kufunga pores ili kuzuia uchafu na mafuta ya ziada yasihitajika kuingia kwenye vishina vya ngozi ya nywele yako(scalp).
✨🌸Hair cuticles zinabaki zimejifunga/zimefungwa zikiosha/kusuuzwa kwa mara ya mwisho na maji ya baridi. Hii hupelekea kuwa na nywele imara ambayo haina mafuta na uchafu mwingi, ambayo hupelekea kuwa na ngozi ya kichwa yenye afya.🧚♂️
0 Comments