Natural Bliss

118. KWA NINI HAISHAURIWI KUSUKA NYWELE KAVU



Kati ya makosa makubwa ambayo watu wengi hufanya katika utunzaji wa nywele ni kublowdry nywelw halafu ndio wanasuka.

☘️Kumbuka ukiblow dry nywele umeondoa unyevu wake wote wa nje na wa ndani hivyo nywele inakua kavu na wakati wa kusuka unaikunja kunja nywele ambapo unaipa tension.

☘️Ukavu wa nywele + Tension (Kuvutwa/Kukunjwa kunjwa) = Kukatika

☘️Watu wengi hulalamika nywele inakatika sana wakati anafumua, hiyo ndio sababu kubwa kusuka nywele ikiwa kavu sana na ambayo imeshakua dhaifu.

☘️Na wengi mnablow dry halafu mkiwa mmesuka mnapaka sana mafuta, butters na bidhaa nyingine za nywele ukidhani unazipa nywele unyevu ila wakati unafumua bado nywele zinakatika. 

KUMBUKA: Hizo hazisaidii sana sana zinaongeza ukavu zaidi na zaidi.


☘️Hata kama hujablow dry nywele, usisuke nywele zikiwa kavu maana nywele haina nguvu kuhimili kuvutwa, kusukwa kubabwa styles nk zikiwa kavu.

☘️Hivyo ukisuka nywele kavu unakua umeongeza tatizo kwenye nywele zako; badala ya kuzipa nywele protective style unakua umezipa nywele UNPROTECTIVE STYLE


💃🏼LEARN&SLAY

Post a Comment

0 Comments