☘️Majani ya mpera yana vitamin B hii ni Biotin nzuri sana kwa nywele.
Bidhaa nyingi za nywele zinaitumia kutokana na faida zake na pia wengne wanameza supplements zenye biotin hii yote ni kuipa nywele nutrients. Majani ya mpera pia yana Vitamins A na C.
☘️ Majini ya mpera kwa nywele yanaweza kutumika kwa aina mbili hair tea na steaming.
1. HAIR TEA.(maana yake huoshi ukisha spray kwenye nywele yako kwenye ngozi na juu)
Kwakua lengo letu ni kuipa nywele zetu unyevu na chai/maji ya mpera ni mazuri kwa hili sababu
➖Inasaidia kuilinda ngozi isipate maradhi kama mba,fungus, infections
➖inarudisha rangi ya nywele ambayo imepotea na wenye mvi pia inakusaidia
➖Inasadia nywele kukua vizuri.
➖inaipa nywele afya.
ni moisturizer nzuri unakua unaspray kisha unapaka mafuta juu hata kama umesuka .
JINSI YA KUANDAA NA KUITUMIA
➖chemsha hayo majana kama unachemsha chai ya rangi
➖Ikichemka iache ipoe then weka kwenye spray bottle .
➖Ukishaspray maji yako paka mafuta kwenye nywele
☘️Hii ni kama chai inakaa salama siku moja au siku mbili bila kuharibika. Iwapo utahifadhi kwenye fridge unaweza tumia wiki nzima.
Haya si matokeo ya siku moja kuona mabadiliko tumia kwa muda mrefu zaidi angalau hata miezi3 na utashuhudia mabadiliko mazuri ya nywele zako.
0 Comments